Tanzania yauza nje nyama tani 10,415 mwaka 2021/2022
Imewekwa: 21 Feb, 2023
Tanzania yauza nje nyama tani 10,415 mwaka 2021/2022

Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Tanzania ilisafirisha jumla ya tani 10,415 za nyama nje ya nchi yenye thamani ya Dola za kimarekani 42,500,994.90. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 492 ikilinganishwa na usafirishaji wa nyama ulio fanyika nje ya nchi mwaka 2020/2021.Qatar ndiyo ilikuwa mnunuzi mkuu wa nyama kutoka Tanzania, ikiwa na tani 3,603 za nyama sawa na asilimia 41 ya nyama iliyosafirishwa nje ya nchi. Maeneo mengine ya usafirishaji wa nyama kutoka Tanzania kama inavyooneshwa katika kielelezo hapo juu