DKT. MUSHI AZINDUA GARI JIPYA LA BODI YA NYAMA
Imewekwa: 11 Jul, 2023
DKT. MUSHI AZINDUA GARI JIPYA LA BODI YA NYAMA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dkt. Daniel Mushi amewapongeza Bodi ya Nyama Tanzania kwa kununua gari jipya litakalorahisisha shughuli za ukaguzi katika tasnia ya nyama.

Dkt. Mushi ametoa pongezi hizo wakati akizindua gari jipya la Bodi hiyo aina ya Toyota Hilux Pickup Double cabin lenye thmani ya zaidi ya shilingi milioni 99. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Bodi hiyo jijini Dodoma, Julai 10, 2023.

Dkt. Mushi ameitaka Idara ya Ufundi  kusimamia vizuri makusanyo ya fedha ili kuweza kufanya mambo mkubwa zaidi ya kuimarisha shughuli za Bodi.

“Niwapongeze idara ya ufundi kwa hayo ambayo mmefanya, mmekuwa mkikusanya fedha muendelee kufanya vizuri zaidi katika ukusanyaji ili Bodi iendelee kukua” amesema Dkt. Mushi.

Gari hilo litakalotumiwa na Ofisi ya Kanda ya Kaskazini inayojumuisha  Mikoa ya Arusha, Tanga, Manyara na Kilimanjaro.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema ana imani Kanda nyingine zilizobakia zitapata pia magari ambazo ni Nyanda za juu Kusini, kanda ya magharibi na kanda ya ziwa.

Awali akiongea na watumishi Dkt. Mushi amewaasa watumishi kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano ili kuweza kuiendeleza Bodi Makao Makuu na kwenye ofisi za Kanda.  Amewasisistiza Idara na Vitengo vyote kufanya kazi kwa moyo ili kuleta matokeo chanya kwenye Bodi.

Naye, Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania Bw. John Chasama akimshukuru Dkt. Mushi amesema Bodi inajivunia yeye katika uongozi wake uliopita kwani  alitengeneza njia bora ya mafanikio ambayo yanaonekana sasa.